Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma (CMT) imetembelea Ujenzi wa Mradi wa Shule ya Sekondari ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Ndg. Philemon Mwita Magesa ametembelea Ujenzi wa Madarasa 22, Maabara nne, Jengo moja la Tehama, Jengo la Maktaba , Ofisi saba za walimu,Nyumba tano za Walimu,Mabweni tisa na Bwalo kubwa la kisasa na ukumbi wa Kulia Chakula.
Magesa amewataka Wakandarasi na Mafundi kufanya kazi kwa Ubora kwa kuzingatia Viwango halisi vilivyowekwa na Ofisi ya Rais Tamisemi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.