BENKI ya CRDB Kanda ya Kusini,imetoa msaada wa meza 40 na viti 40 vyenye thamani ya Sh.milioni tatu katika shule ya Sekondari Kungu iliyopo kata ya Nakayaya Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Meneja wa CRDB Kanda ya Kusini Daniel Mwoleka amesema,wameamua kutoa msaada huo ili kurudisha faida kwa wadau wake kwani kuna kila sababu ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali.
“Benki ya CRDB kama mdau mkubwa wa elimu tunayo furaha kuwepo mahali hapa kwa ajili ya kutoa mchango wetu kwa ajili ya shule hii,kama nilivyosema sisi ni mdau wakubwa wa elimu”alisema Mwoleka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Ismail Hamis Seleman, ameishukuru benki ya CRBD kwa msaada huo ambao utapunguza uhaba wa vifaa katika shule hiyo ambayo ina miaka miwili tu tangu kuanzishwa kwake.
Mkuu wa shule hiyo Ayoub Kundya amesema,kilichofanywa na Benki ya CRDB ni jambo kubwa kwani mahitaji ya vifaa kwa ajili ya wanafunzi ni makubwa na watakuwa mabalozi wazuri wa benki hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.