Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ilitoa shilingi bilioni 1.55 ili kurejesha sehemu yake daraja la Muhuwesi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
Daraja hilo lilipata hitilafu kutokana mvua za masika kwenye mto Muhuwesi katika mwaka 2023
Kabla ya marekebisho hayo magari yalikuwa yanapita upande mmoja ambapo hivi sasa magari yanapita pande zote mbili.Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Saleh Juma alisema,kwa sasa daraja hilo ni salama na haliwezi kusogea tena kama ilivyotokea hapo awali, na amewatoa hofu watumiaji hasa wenye magari kuhusu uimara wa daraja hilo linalounganisha mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.