Mdahalo wa kuadhimisha Siku ya Mashujaa umefanyika leo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, wilayani Namtumbo, ukihudhuriwa na viongozi, wazee, na wananchi kwa ujumla.
Mgeni rasmi katika mdahalo huo alikuwa Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Ndugu Francis Mgoloka . Katika hotuba yake,
Mgoloka alitambua jitihada za wazee waliopambana kwa ajili ya uhuru wa Tanzania na kusisitiza umuhimu wa kuenzi mchango wao kwa maendeleo ya taifa.
Mdahalo huo ulilenga kujadili namna mbalimbali ambazo mashujaa walishiriki katika harakati za ukombozi wa nchi. Aidha, Mgoloka alieleza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo ipo tayari kushirikiana na wadau katika kutafuta historia ya Chief Mkomanike, mmoja wa mashujaa wa ukombozi wa nchi.
Katika kuenzi historia na tamaduni za taifa, mgeni rasmi aliongoza matembezi ya kukagua vifaa vya kale, ikiwa ni pamoja na vyakula vya asili, tiba za kienyeji, na silaha zilizotumiwa na mababu zetu katika harakati mbalimbali za kujihami.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.