Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe Ngollo Malenya amewataka Wakulima wilayani umo kuacha kuwatumia Watoto kama vibarua mashambani
Akitoa maagizo hayo katika kikao cha kawaida cha mwaka cha Wajumbe wa chama kikuu cha ushirika Songea-Namtumbo (SONAMCU) kilichofanyika hivi karibuni ukumbi wa Chndamali Mjini Songea
Malenya amesema ajira kwa watoto ni makosa kwani hata sheria za nchi zinasema mtoto anapaswa kulinda na sio kumtumikisha kwahiyo wazazi watakao kutwa wanafanya hivyo sheria zitachukuliwa haraka iwezekanavyo
“Hili limekuwa likilalalamikiwa sana kwamba wazazi wengine wamekuwa wakiwatumikisha watoto katika mashamba yao hilo kwenye serikali alikubaliki kwenye kanuni na sheria ndogo ndogo haikubariki”
Hata hivyo Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka, 2004 kinamuelezea mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 14 isipokuwa kwa ajira zilizo katika sekta hatarishi, mtoto maana yake ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.