Mkuu wa Wilaya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo ameiagiza Kampuni ya Uchimbaji madini ya makaa ya mawe TANCOAL kufanya uthamini upya wa athari za nyumba zilizoharibika kutokana na mlipuko wa baruti ili kuwalipa fidia wananchi wa Ntunduwaro.
Mangosongo ametoa maagizo hayo Wakati anazungumza na wananchi wa kijiji cha Ntunduwalo kata ya Ruanda Halmashauri ya Mbinga.
Wananchi wa kijiji hicho walipata athari za uharibufu wa mali na nyumba kutokana na milipuko wa baruti uliofanywa na Kampuni ya uchimbaji madini ya TANCOAL.
Wananchi wa Ntunduwaro Awali waliwasilisha malalamiko katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga kuhusiana na athari hizo hali uliyosababisha Mkuu wa Wilaya kufanya ziara.
Wakizungumza kwenye mkutano huo wananchi wamedai uwepo wa milipuko karibu na makazi ya watu na kusababisha Uchafuzi wa mazingira hasa katika vyanzo vya maji.
Baada ya kusikliza kero za wananchi Mkuu wa Wilaya ameiagiza Idara ya Ardhi na Kamati ya CSR kufanya tathmini ya nyumba ambazo zimeharibiwa,Kisha Mgodi ulipe fidia za athari hizo.
Ametahadharisha kuwa mgodi ukishindwa kulipa fidia wasitishe uchimbaji katika eneo hilo na kwenda kufanya uchimbaji eneo jingine.
“Natoa mwezi mmoja mgodi na wananchi kukubaliana namna ya kuwafidia Pia nataka zoezi la uthamini lifanyike ndani ya siku saba tu",alisisitiza Mangosongo.
Mkuu wa Wilaya ameziagiza Kampuni zote zinazochimba Madini ya makaa ya mawe kutekeleza CSR kadiri ya makubaliano kwenye vipaumbele vya kila kijiji.
Ameziagiza kampuni hizo kutoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka mgodi.
Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Mgodi wa TANCOAL Mhandisi Enock Mwambeleko amekiri kuwepo kwa milipuko iliyosababisha uharibifu ambapo ameahidi kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya kwa wakati.
Mwakilishi wa Afisa Madini Mkoa Yese Mkimbi ameiagiza kampuni ya TANCOAL na Kampuni nyingine za uchimbaji madini kuwasilisha mpango kazi wao katika ofisi za madini mkoa ili nyaraka hizo zipitiwe na kuridhiwa kama mikakati ya kufanya ulipuaji imekidhi vigezo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.