• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC Mbinga awaonya wakandarasi wababaishaji

Imewekwa kuanzia tarehe: February 7th, 2023

MKUU wa wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo,amezitaka taasisi zinazosimamia sekta ya ujenzi wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) na Tarura,kutowapa kazi wakandarasi wabovu na wenye Historia mbaya ya kujenga na kukarabati barabara chini ya viwango.

Amesema,wakandarasi  hao wanasababisha hasara kubwa kwa serikali kwa kuwa inalazimika kufanya matengenezo ya barabara mara kwa mara na kutumia fedha nyingi ambazo zingepelekwa kujenga miradi na kuboresha huduma nyingine za kijamii.

Badala yake Mangosongo,ameitaka TANROADS na Tarura, kuwapa kazi wakandarasi walioonyesha uwezo mkubwa katika ujenzi wa miradi ya barabara wakiwemo  makundi ya vijana na wanawake waliopata mafunzo ya kujenga miradi  ya  barabara.

Mangosongo ametoa kauli jana,wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi kwa vikundi vya wanawake na vijana wilayani Mbinga yaliyotolewa na taasisi ya teknolojia ya ujenzi ICOT-Mbeya.

Amesema,vijana  hao kama watatumika vizuri watakuwa msaada mkubwa kwa serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za wilaya na mkoa wa Ruvuma kwa gharama nafuu,badala ya kuwatumia wakandarasi wababaishaji,wasiokuwa na uwezo na uzalendo kwa nchi yao.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya,amewaasa vijana hao  kwenda kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ili waweze kupewa miradi mingi na hivyo kukuza fani ya ukandarasi katika sekta ya ujenzi wa barabara na hata majengo.

“nawahakikishia serikali ya wilaya,itakuwa bega kwa bega na nyinyi ili mafunzo haya mliyoyapa yakatumike kikamilifu katika miradi ya ujenzi wa barabara katika wilaya yetu ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma  na kuwakomboa kiuchumi”alisema Mangosongo.

Katika hatua nyingine Mangosongo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo,ameziagiza Halmashauri za wilaya ya Mbinga na Halmashauri ya Mji Mbinga kuwapa mikopo vijana hao kama njia ya kuwajengea uwezo ili waweze kutumia elimu waliopata kukuza uchumi binafsi wilaya na Taifa.

Ametoa ushauri kwa Halmashauri hizo,kuwa na utaratibu wa kuwapa elimu ya ujasiriamali kwanza kabla ya kutoa mikopo kwa vikundi  ili fedha zinazotolewa ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa ya kuwaondolea wananchi waliojiunga kwenye vikundi  na umaskini,badala ya kutumika kinyume na malengo ya serikali.

Kwa upande wao washiriki waliohitimu mafunzo hayo kupitia risala iliyosomwa na Betram Kapinga,wameiomba serikali kuwapa fursa zaidi katika kazi za ujenzi wa barabara ili kuwajengea uwezo na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi binafsi na Taifa.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Contruction Ltd Valence Urio, amewataka wahitimu hao kuwa waadilifu,waaminifu,kuwa na uthubutu na kutanguliza maslahi ya Taifa wanapotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara  badala ya kutanguliza maslahi binfasi.

Jumla ya vijana 17 kati yao wanaume 11 na wanawake 6 wameshiriki katika mafunzo hayo, yenye lengo la kuwawezesha vijana wakandarasi waliojiunga kwenye vikundi kushiriki katika ujenzi wa barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.