• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC MBINGA awaonya watumishi kuacha matumizi ya fedha mbichi

Imewekwa kuanzia tarehe: February 14th, 2023

WATENDAJI wa vijiji na kata katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wamelazimika kula kiapo cha uaminifu na uadilifu kwa ajili ya kwenda kukusanya  na kusimamia mapato ya serikali.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya watumishi waliopewa jukumu ya kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo ikiwamo kituo(geti) la Kitai  linalokusanya ushuru wa malori yanayobeba makaa ya mawe na mazao kudaiwa  kujihusisha na wizi kwa kutopeleka  sehemu ya fedha hizo  benki kama inavyotakiwa.

Akizungumza baada ya kiapo  hicho,Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Mheshimiwa Aziza Mangosongo,amewaonya watendaji na watumishi  wengine kujiepusha na matumizi ya fedha mbichi zinazokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya mapato.

Badala yake, wahakikishe wanaisaidia serikali kukusanya mapato  na maduhuli mengine na fedha zote zinazokusanywa zinapelekwe benki na sio vinginevyo.

Amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo, kuhakikisha wanasimamia eneo la ukusanyaji wa mapato ili kuiwezesha Halmashauri kutekeleza miradi itakayoleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Mangosongo ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki, wakati akizungumza na watumishi  wa Halmashauri hiyo kwenye kikao kazi cha wadau wa makaa ya mawe kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Kigonsera.

Amewasisitiza kufanya kazi kwa weledi,kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo kwa uadilifu na uaminifu ili miradi hiyo ilingane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na serikali.

Katika hatua nyingine Mangosongo,amewakumbusha madiwani ambao ni wajumbe wa kamati ya fedha,kuwa na utaratibu wa kutembelea na kukagua miradi mara kwa mara ili kujiridhisha juu ya ufanisi wake badala ya kusubiri kupokea taarifa za wataalam.

Mangosongo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Mbinga,amemuagiza mweka hazina wa Halmashauri  na watumishi wanaokusanya mapato kujipanga ili kutafuta namna bora ya kuongeza mapato.

Awali Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wilaya ya Mbinga Blandina Hamis alisema,uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo umebaini kuwa,baadhi ya  madereva wa malori yanayobeba makaa ya mawe hawalipi kiwango cha fedha kilichopangwa cha Sh.30,000 yanapopita geti la Kitai.

Alisema kuwa,kuna magari yanalipa fedha ndogo kati ya Sh.20,000,15,000 na 1,000 na kupewa listi ya  kubeba mazao badala ya makaa ya mawe na mengine hayakatiwi listi,bali madereva wanalipa fedha kwa njia ya simu za wafanyakazi wa getini ,hivyo kuikosesha serikali mapato.

Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Mbinga Frederick Msae alisema,idadi ya malori yanayobeba makaa ya mawe na kupita katika geti la Kitai ni  300 hadi 450 na mapato yalikuwa Sh.milioni 2  hadi milioni 4 kwa siku.

Alisema, baada ya Takukuru kustukia mchezo mchafu unaofanywa na watumishi waliopewa dhamana ya kukusanya ushuru na kufanya uchunguzi wa kina  sasa mapato yameongezeka  hadi kufikia Sh.milioni 10.

Kwa upande wake Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Samweli Marwa,amehaidi kuongeza udhibiti wa upotevu wa mapato katika geti la Kitai  na maeneo mengine.

“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya mimi na watu wangu tutajipanga upya kudhibiti upotevu  wa mapato katika geti hili”alisema Marwa.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.