Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Mbinga imefikia asilimia 83.2 ya malengo ya usajili wa watu 223,657.
Hayo yalisemwa wakati wa Uzinduzi wa zoezi la siku 14 la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa Wilaya ya Mbinga, katika tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Aziza Mangosongo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Afisa Usajili Mwandamizi wa NIDA Bw. Ibrahim Liduke alisema hadi Novemba 30, 2023 idadi ya watu waliosajiliwa ilikuwa 185,986.
Alisema kwa sasa watagawa vitambulisho vya Taifa 131,181 ambavyo vimezalishwa hivi karibuni kwa Wananchi na Wakazi wa Wilaya ya Mbinga.
Zoezi hili la ugawaji wa vitambulisho litafanyika kwa utaratibu wa kuvisambaza hadi ngazi ya kata na kukabidhiwa Mtendaji Kata kabla ya kuvikabidhi kwa watendaji wa Mitaa na Vijiji ambao ndio watakuwa na jukumu la kuvigawa kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Aziza aliwataka watendaji kata wawahamasishe wananchi kujitokeza kwa wingi kufuata vitambulisho vyao.
na kwamba Ugawaji wa vitambulisho utakata kiu ya muda mrefu ya wananchi wa Wilaya ya Mbinga waliokuwa wakisubiri vitambulisho vyao kwa muda mrefu,” alisema Mhe. Aziza.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.