Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma Mhe. Kisare Matiku Makori, amezindua rasmi kampeni ya upandaji miti katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Lusonga.
Kampeni hiyo, iliyoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa kushirikiana na Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira cha Halmashauri ya Mji wa Mbinga, inalenga kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira.
Akihutubia katika uzinduzi huo, Mhe. Makori alisisitiza umuhimu wa upandaji miti kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia alihimiza wananchi kuachana na tabia hatarishi kwa mazingira, kama uchomaji miti na matumizi ya mkaa, na badala yake kutumia nishati safi ya kupikia.
“Wale wenye utaratibu wa kuhujumu mazingira kwa kufanya vitendo vilivyokatazwa kisheria wanapaswa kubadilika ili tushirikiane kutunza mazingira,” alisema Mhe. Makori.
Aidha, aliwataka wananchi kutumia kipindi hiki cha mvua kupanda miti na maua katika maeneo ya umma na nyumbani kwao ili kuimarisha uhifadhi wa mazingira.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.