• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

DC MTATIRO asikiliza kero za wafanyabiashara soko la Tunduru

Imewekwa kuanzia tarehe: June 13th, 2023

BAADHI ya wafanyabiashara katika soko la Azimio wilayani Tunduru,wamelalamikia kukithiri kwa vitendo vya wizi na udokozi wa bidhaa zao jambo linalorudisha nyuma jitihada za kujitafuta kipato na kukuza uchumi wa familia na Taifa.

Wakizungumza  mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Wakili Julius Mtatiro walisema,vitendo hivyo vinafanywa na walinzi wanaoshirikiana na vibaka wanaoingia ndani ya soko na kuiba bidhaa mbalimbali.

Kassim Makasi alisema, matukio hayo yanatokea nyakati za usiku kwa kuwa mageti ya soko ni mabovu na baadhi ya walinzi waliowekwa na Halmashauri wanafika kazini wakiwa wamelewa na wengine wazee,hivyo ni rahisi vibaka kuingia ndani na kufanya uharifu jambo linalo wasababishia hasara kubwa.

“mara kwa mara mafundi wanakuja kuchukua vipimo kwa ajili ya kutengeneza mageti mapya lakini tunasikitika sana tangu mwaka jana hakuna kilichotekelezwa,tunakuomba Mkurugenzi weka mageti mapya ili yatusaidie ulinzi wa bidhaa zetu”alisema Makasi.

Aidha alisema,baadhi ya walinzi siyo waaminifu na wanahusika  moja kwa moja kuiba bidhaa zao na kuiomba  Halmashauri kuwafukuzwa  katika soko hilo ili wapatikane walinzi wengine watakaosaidia kuimarisha ulinzi.

Ali Bakari, amelalamikia huduma mbovu ya vyoo kwani matundu yaliyokuwepo ni machache,na wanalazimika kwenda maeneo mengine nje ya soko kupata huduma hiyo.

Alisema soko hilo ni sehemu ya mapato  kwa Halmashauri,hivyo ni muhimu  serikali kuimarisha miundombinu yake badala ya kukimbilia kuchukua fedha za pango na ushuru kutoka kwa wafanyabiashara.

Zaitun Ahmad alisema,wafanyabiashara wa soko hilo wako katika hatari ya kupata magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindu pindu,kuharisha na magonjwa ya tumbo kutokana na kukosekana kwa  huduma ya maji safi na salama.

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wilayani Tunduru Efrem Mbwilo alisema,Halmashauri ya wilaya imepora baadhi ya vibanda vilivyojengwa na wafanyabiashara na kuwapa watu wengine.

Alisema kisheria vibanda hivyo ni  vya Halmashauri,lakini vimejengwa na wafanyabiashara ambao ndiyo wamiliki halali kwa hiyo Halmashauri haikupaswa kuwapora,badala yake ilitakiwa kukaa nao ili kuingia makubaliano mapya.

 “Halmashauri haijawahi kujenga vibanda katika soko hili,vibanda vyote vimejengwa na watu  na wafanya biashara wamenunua kutoka kwa wamiliki wa awali”alisema Mbwilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Chiza Marando amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kueleza kuwa,kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imetenga  kiasi cha fedha zitakazotumika kufanya ukarabati  wa soko na kuboresha huduma zake ikiwemo maji na vyoo.

Akizungumzia changamoto ya kukithiri kwa uchafu sokoni hapo alisema,tayari wamefanya matengenezo ya lori moja na kutenga fedha kwa ajili ya kununua lori jipya ambayo yatafanya kazi ya kuzoa taka siyo katika soko tu bali katika maeneo yote mji wa Tunduru.

Pia,amewataka wafanyabiashara kulipa kodi  za vibanda kwa wakati ili kuepuka usumbufu au kulazimika kulipa faini kubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro ametoa wiki mbili kwa Halmashauri ya wilaya kuhakikisha ina Imarisha ulinzi kwa kujenga mageti mapya na kuboresha huduma ya vyoo na maji katika soko hilo.

Alisema,malalamiko yote ya wafanyabiashara yana ukweli na kama Halmashauri itashindwa kutatua kero hizo kutokana na mamlaka aliyonayo anaweza kuamuru wafanya biashara wasilipe pango za vibanda wala ushuru kwa muda wa miezi sita ili fedha hizo zitumike kuimarisha ulinzi na huduma muhimu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.