Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Mhe. Ngollo Malenya, akiambatana na Kamati Usalama ya Wilaya,, ametoa maagizo ya kukamilishwa kwa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Namtumbo ndani ya siku saba.
Mradi huo wa bweni umegharimu shilingi milioni 100, fedha zilizotolewa na Serikali Kuu kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mhe. Malenya amesisitiza kuwa wanafunzi wote wenye mahitaji maalum wanapaswa kukaa bweni ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya kusomea na kuishi.
Aidha, ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu bora bila vikwazo vyovyote.
Amewataka viongozi wa Halmashauri kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa kwa wakati ili kufanikisha dhamira ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.