Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhe. Ngollo Malenya, amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mbegu Tanzania (TARI), Dkt. Thomas Bwana, kujadili juhudi za kuboresha sekta ya kilimo kupitia uzalishaji wa mbegu bora.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Malenya amepongeza kazi kubwa inayofanywa na TARI na kusisitiza ushirikiano wa serikali katika kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora zenye tija.
Dkt. Bwana ameweka wazi kuwa TARI inahusika na utafiti wa mbegu mbalimbali, zikiwemo za asili na za kisasa, huku akieleza kuwa wakulima wengi wanapendelea mbegu za kisasa kwa sababu ya uzalishaji mkubwa wa mazao.
Aidha, amefafanua kuhusu shamba la utafiti wa mbegu lililopo Suluti, ambapo majaribio yanafanyika kwa mazao kama ufuta, mbaazi, mahindi, na karanga. Ametaja kuwa zaidi ya aina 100 za mbegu za mahindi zinafanyiwa utafiti ili kubaini zile zenye tija zaidi kwa wakulima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.