Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Mhe. Ngollo Malenya, ameongoza zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Vita Kawawa, Suluti, kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Tukio hilo limekusudia kuhamasisha utunzaji wa mazingira na ushiriki wa wanawake katika maendeleo endelevu.
Wanawake mbalimbali kutoka wilayani Namtumbo walihudhuria shughuli hiyo, wakionesha mshikamano wao katika kulinda mazingira.
Zoezi hilo liliibua mjadala kuhusu nafasi muhimu ya wanawake katika kutunza mazingira na kuhakikisha ustawi wa vizazi vijavyo.
Katika hotuba yake, Mhe. Ngollo alisisitiza jukumu la wanawake katika kuhifadhi mazingira.
Alisema kuwa wanawake ni nguzo muhimu ya maendeleo na mchango wao katika upandaji miti ni wa thamani kubwa kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.