Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhe. Ngollo Malenya, ameongoza kikao muhimu na wenyeviti wa vitongoji na vijiji, akiwataka kufanya kazi kwa uadilifu na kutunza nyaraka muhimu za ofisi, hasa zinazohusu masuala ya ardhi, ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
Kikao hicho, kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kilihusisha pia wawakilishi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa, Ombolo, kwa lengo la kuwawezesha viongozi wapya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Katika hotuba yake, DC Malenya alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira, akibainisha faida zake za kiuchumi, kama biashara ya hewa ukaa (carbon trading). Alisema suala hilo ni moja ya ajenda kuu zinazosisitizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, aliwataka viongozi wa vijiji na vitongoji kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira, kulinda rasilimali za umma, na kuwajibika ipasavyo kwa wananchi.
Kikao hicho kinalenga kuongeza uwajibikaji wa viongozi wa ngazi za msingi ili kuhakikisha huduma za serikali zinawafikia wananchi kwa ufanisi na kuimarisha utawala bora.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.