Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imeandaa kongamano maalumu kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, likiwakutanisha wanafunzi wa kike kutoka Shule za Sekondari za Limbo, Mbamba Bay, na Lovund pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Nyasa.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa VETA Nyasa, likihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Magiri amesisitiza umuhimu wa wanawake kuimarisha familia zao kwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Ameeleza kuwa jamii inamtegemea mwanamke katika kujenga usawa, kukuza uchumi, kuimarisha maadili mema, na kudumisha ndoa imara.
Aidha, amesisitiza kuwa mwanamke bora ni yule anayewalea watoto wake vyema kwa kuwapatia huduma na elimu bora.
Mhe. Magiri ametoa wito kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa jamii kwa kujitokeza kugombea nafasi za udiwani na ubunge, hasa kwa kuwa mwaka 2025 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu.
Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zilitolewa, zikiwemo elimu juu ya ukatili wa kijinsia, hedhi salama, sheria ya ndoa, pamoja na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi, ili kuboresha afya na ustawi wa watoto wa kike.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.