Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas amepiga marufuku mavazi yasiyo na staa katika Wilaya ya Nyasa, na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Nyasa kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote wanaovaa mavazi yasiyokuwa na maadili.
Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akiongea na kujibu Kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo ,Kata ya Tingi Wilayani Nyasa.
Aidha amekemea tabia ya Wanaume wanaopiga wake zao, na kuwaambia wabadilike, Vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria .
Ameongeza kuwa watu wa Wilaya ya Nyasa ni wastaarabu na wanatakiwa kuwa na amani muda wote, na kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi yanayokubalika katika Jamii.
Ameongeza kuwa nguo fupi kwa wanawake hazitakiwi na Sururali zilizoshuka kiunoni maarrufu kama Mlege, hazitakiwi Wilayani Nyasa.
"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza nguo zao zinakuwa nadhifu. Nguo fupi na Milege Hazitakiwi Wilayani Nyasa".
Habari imeandikwa na Netho Credo
Afisa Habari Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.