Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri, ameshiriki uzinduzi wa Mradi wa Jamii Shirikishi Katika Uzalendo na Ulinzi utakaotekelezwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Global Peace Foundation chini ya ufadhili wa Serikali ya Uholanzi. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 18 Februari 2025.
Mradi huu wa mwaka mmoja utatekelezwa katika Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, na Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.
Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Sea View Resort, mjini Lindi, na kuhudhuriwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Wiebe de Boer pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.