Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mheshimiwa Peres Magiri, amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kushiriki kikamilifu Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu 2024.
Ameyasema hayo wakati anazungumza na wananchi katika Kijiji cha Ndengere Kata ya Mbambabay ambapo pia alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa wananchi, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Magiri amewaeleza wananchi hao kuwa mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wananchi, wanatakiwa kushiriki kwa kujitokeza kugombea na kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.
“Ushiriki wa wananchi ni muhimu sana Katika Uchaguzi wa mwaka huu ili kuchagua viongozi bora, ngazi ya chini ambao watapunguza malalamiko na kero za wananchi katika Ngazi ya Vijiji na Kata’’,alisisitiza.
Ametoa rai kwa makundi maalum kama wanawake,wenye ulemavu na vijana kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa mwaka huu,ikiwa ni Pamoja na kuchukua fomu za kugombea nafasi za Uongozi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa anafanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika kata za Mbambabay na Mbaha kwa lengo la kuzungumza na wananchi na kusikiliza kero zao
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.