Mkuu wa wa Wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba, amewataka wananchi Wilayani hapa,kushirikiana na kutatua Changamoto zinazowakabili hasa za Ujenzi wa Miundombinu ya Shule bila kuisubiri Serikali.
Ameyasema hayo jana wakati akiweka Jiwe la Msingi, katika Shule mpya ya Sekondari Luhangarasi , na Kukabidhi Cheti cha Usajili kwa Uongozi wa Kata Ya Luhangarasi Tarafa ya Mpepo, Wilayani Nyasa.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo Mkuu huyo, amewapongeza wananchi, kwa kushiriki kikamilifu ujenzi wa Miundombinu ya Madarasa manne, Jengo la Utawala na matundu nane ya Vyoo yaliyotumia zaidi ya Sh Milioni 60, Zilizochangwa na wananchi , kwa Lengo la Kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari, katika Kata hiyo na kuwalazimu wanafunzi kutembea umbali wa km 09 kufuata Sekondari katika Kata jirani ya Kingerikiti.
Chilumba amefafanua kuwa, wananchi wa Kata ya Luhangarasi ni Mfano wa kuigwa katika Wilaya ya Nyasa, kwa kuwa mara baada ya kuona wana tatizo la ukosefu wa shule ya Sekondari waliamua Kushirikiana na kujenga Shule yao kwa Asilimia mia moja, bila kuisubiri Serikali.
Aidha ametoa wito kwa Wananchi wa Wilaya ya Nyasa Kuiga Mfano huu, wa kujitatulia matatizo yao wenyewe ili kujiletea maendeleo kwa haraka.
Awali akisoma Taarifa ya Shule hiyo Kaimu Afisa Mtendaji Wa Kata hiyo amesema Ujenzi huo ulianza mwaka 2019 kwa vikao halali na vilivyowashirikisha wananchi, wakakubali kutatua changamoto ya watoto wao kutembea Umbali wa km 09 kufuata Shule, hali iliyokuwa ikiwapa usumbufu mkubwa kuweza kufuatilia maendeleo ya shule.
Aidha wananchi hao wameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Nyasa, kwa juhudi zao za kuhakikisha shule hiyo inapata namba ya Usajili namba S.5524 Luhangarasi sekondari na kuwapeleka wanafunzi kuanza masomo katika shule hiyo mapema mwaka huu 2021, kwa wanafunzi 188 wa Kidato cha kwanza kudahiliwa, shuleni hapo.
Naye Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Nyasa Mwl Rogers Semwalekwa , amewapongeza wananchi hao kwa kutatua changamoto ya ukosefu wa Shule, na ameunga mkono kama Halmashauri kwa kutoa Vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya Tsh 1,200,000, pia tayari shule imeingizwa kwenye mfumo wa malipo ya Pranrep kwa ajili ya kupewa Fedha za ruzuku za elimu bila malipo, kutoka Serikalini, na tayari akaumti ya Shule imefunguliwa, na kuendelea kutatua changamoto mbalimbali Shuleni hapo ili kuunga mkono jitihada za wakazi wa Luhangarasi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Bw. Jimson Mhagama amewapongeza wananchi hao na kuwataka kuendeleza juhudi hizo ili kutatua changamoto zingine na kuwaahidi Serikali inaendelea kushughulikia Utatuzi wa Changamoto zingine zinazoikabili shule hiyo.
Imeandikwa na Afisa Habari Wilaya ya Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.