Mkuu wa Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile, ametoa maelekezo kwa wataalamu wa Manispaa ya Songea kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya stendi ndogo ya Ruhuwiko ili kuimarisha huduma kwa wananchi.
Ndile ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kushitukiza katika eneo hilo, ambapo alibaini changamoto kadhaa zinazohitaji kutatuliwa haraka.
Changamoto hizo ni pamoja na ukarabati wa choo cha kulipia kinachosimamiwa na Halmashauri, ujenzi wa kibanda cha kukaa abiria wakati wanasubiri usafiri, na ukosefu wa maji safi katika eneo hilo.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Ndile ameagiza changamoto hizo zitatuliwe ndani ya muda wa wiki moja.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliongozana na wataalamu wa Manispaa ya Songea
Ziara hiyo inatarajiwa kuchochea maboresho ya haraka katika stendi ya Ruhuwiko ili kuboresha huduma kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa miundombinu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.