Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile amewataka Maafisa Watendaji Kata, Mitaa, Waratibu Elimu Kata, na Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari wilayani humo kutoa ushiririkiano wa kutosha katika kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza, awali na darasa la kwanza wanaripoti shule.
Ndile ametoa agizo hilo katika kikao kazi cha kuhakiki takwimu za wanafunzi walioripoti shule kuanzia awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa wanafunzi hao.
Amewaagiza maafisa watendaji kuhakikisha kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2024 awe ameripoti shule na mzazi yeyote atakayeshindwa kupeleka mtoto wake shule achukuliwe hatua za kisheria.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.