MKUU wa Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile, ametoa ushauri kwa Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi nchini kutafakari upya kuhusu uwepo wa zaidi ya chama kimoja cha wafanyakazi wa kada moja.
Amesema hali hiyo inasababisha migogoro na migongano kazini, jambo linalochangia kushuka kwa nidhamu katika sekta ya elimu.
Ndile alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana mjini Songea.
“Heshima ya walimu kwa sasa imeshuka kutokana na mgawanyiko huu. Wamekuwa na makundi mawili yenye misimamo tofauti, hali inayochangia kushuka kwa nidhamu sehemu za kazi,"alisema Ndile.
Amewasihi walimu kuungana na kuwa kitu kimoja badala ya kuendelea na migawanyiko inayodhoofisha mshikamano wao.
Awali, Katibu wa CWT wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Adriano Ngairo, alisema walimu 255 wamefukuzwa uanachama kwa kwenda kinyume na maadili ya chama hicho.
Pia, alisema katika kipindi cha miaka minne, walimu 440 wamepandishwa madaraja kulingana na mwongozo wa serikali.
Aliishukuru serikali kwa maboresho hayo ambayo amesema yamechangia kurudisha morali ya kazi kwa walimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.