Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mheshimiwa Kapenjama Ndile, amesema wanawake wana haki ya kuheshimiwa, kusikilizwa pamoja na kumiliki mali kama ilivyo kwa wanaume.
Ameyasema hayo wakati akifanya uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya wanawake mkoa wa Ruvuma ambapo uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa soko kuu la Songea, huku kilele cha maadhimisho hayo ni machi 8 kimkoa na yatafanyika katika uwanja wa majimaji mjini Songea.
Amebainisha kuwa usawa na haki za mwanamke zipo na zinajulikana, ambapo amesema mwanamke ana haki ya kuishi, kuheshimiwa, kusikilizwa, kumiliki mali na haki ya kuwa na madaraka kama ilivyo kwa mwanaume.
Amewataka wanawake kukataa kuonewa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwa taifa bila haki halitakuwa na utulivu kwa kuzingatia katiba ya nchi ambayo inawataka wananchi kuimarisha usawa wa kijinsia ili kuleta maendeleo kupitia rasilimali za nchi ili kuyanufaisha makundi yote.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Wanawake Mkoa wa Ruvuma, Siwazuri Mwinyi, amesema kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mpaka sasa wamefanikiwa kufanya shughuli mbalimbali katika jamii ikiwemo kufanya harambee kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji na kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalumu.
Pia wametembelea mashuleni kuongea na kugawa taulo za kike wa wanafunzi, kufanya makongamano mbalimbali ya wanawake ambayo yalilenga utoaji wa elimu kwa wanawake pamoja na kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.