Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Mheshimiwa Simon Kemori Chacha, amewaagiza viongozi katika kata na vijiji, pamoja na maafisa elimu kata kuhakikisha wananfunzi wanapata mlo wakiwa shuleni wakati wa masomo.
Amesema kuwa kufanya hivi kutaongeza ufanisi na umakini kwa wanafunzi katika masuala ya elimu, hasa katika kuongeza uelewa pale wanapofundishwa na walimu wao.
“Lishe ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mwanadamu , tunatakiwa kulichukulia hili suala kwa uzito wake katika maeneo yetu tunayoishi”.Alisema Chacha.
Chacha ametoa agizo hili wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe ngazi ya wilaya. Kikao hicho kilihudhuriwa na watendaji wa kata pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Mkuu wa Wilaya amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa kata na vijiji, maafisa elimu, na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha wanafunzi wanapata mlo bora shuleni. Alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kufanya kazi ya kuendeleza lishe bora katika Wilaya ya Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.