MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo BOOST.
Hayo amesema katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano katika ofisi ya Mkurugenzi.
Mohamedi amesema Serikali imeleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Joseph Mhagama shilingi Milioni 470 ambayo imekamilika na imsajiliwa na imeanza kutoa huduma kupitia mradi wa SEQUIP,Shule ya Msingi Lipupuma imekamilika kupitia mradi wa BOOST imejengwa kwa shilingi Milioni 331 na Shule ya Sekondari Lilondo ambayo inajengwa kwa shilingi Milioni 560 na imeanza hatua za kusajiliwa.
“Nichukue fursa hii kumshukuru Mh.Rais kwa kutatua changamoto za Madarasa kwa ujenzi wa Mradi wa Boost hasa madarasa ya awali na darasa la kwanza”.
Mkurugenzi ametoa rai kwa Madiwani kuhakikisha wanawahamasisha wazazi kuandikisha watoto kwa wingi ikiwa Madarasa yamekamika na kuanza kutoa huduma ifikapo Disemba 2023.
Hata hivyo Mohamed amesema kuhusu kidato cha kwanza wamejipanga ikiwa baadhi ya maeneo kulikuwa na upungufu wa madawati Mbunge wa Jimbo la Madaba amesapoti kupitia mfuko wa Jimbo,shule ya Sekondari Matetereka na Joseph Mhagama.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.