Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura ameendelea kutoa msisitizo juu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa Shule zote za Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga akisisitiza kuwa ni Sera ya Serikali katika kutunza mazingira.
Mkurugenzi Kashushura ametoa rai hiyo katika tafrija fupi ya utoaji wa tuzo za taaluma kwa shule za Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Amesisitiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina makaa ya mawe ambayo hutumika kuzalisha mkaa mbadala ambao ni mojawapo ya nishati safi ya kupikia hivyo amewataka walimu hao kutumia fursa hiyo ambayo wengi wanatamani kuwa nayo.
"Haiwezekani tuna rasilimali katika eneo letu alafu bado tuna shangaa shangaa itafikia pointi watu wengine watatoka katika maeneo mengine kuja kuchukua mzigo huku"Amesema
Kwa upande wake Kaimu Afisa Maliasili na Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Chrispine Haonga ameeleza kuwa Halmashauri imeendelea kutoa elimu na kuhamasisha Jamii juu ya matumizi ya nishati safi za kupikia.
Ikumbukwe Julai 11, 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ilikabidhi tani 10 za mkaa mbadala utokanao na makaa ya mawe kwa shule za msingi 15 na Shule za Sekondari 15.
Akithibitisha faida za matumizi safi ya nishati za kupikia Padre Chistopher Mapunda Mkuu wa Seminari ya Likonde ameeleza kwa miaka mingi Seminari ya Likonde ilikuwa inatumia kuni kwa ajili ya kupikia hatua ambayo ilipelekea uharibifu wa misitu lakini kwa sasa Shule inanufaika na matumizi ya nishati ya mkaa mbadala wa makaa ya mawe.
Kwa upande wa Shule ya Sekondari Kigonsera Makamu Mkuu wa Shule Joseph Komba ameeleza kuwa kwa sasa shule hiyo imendokana na matumizi ya kuni kwa ajili ya kupikia na badala yake shule inatumia nishati ya gesi pamoja na nishati ya makaa ya mawe.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.