Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Joseph Rwiza amewataka Walimu Wakuu wa shule za Msingi na Wakuu wa shule za Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuhakikisha wanaweka kisanduku cha huduma ya kwanza( First Aid Kit) shuleni ili kuwezesha utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanafunzi.
Agizo hilo limetolew katika kikao kazi cha Mkurugenzi Mtendaji na walimu Wakuu na Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Tarafa pamoja na Watendaji wa Kata.
" Uwepo wa first aid kit katika shule zetu ni muhimu sana katika kutoa huduma ya kwanza kwa wanafunzi wetu pindi dharula inapotokea ,kwahiyo kila Mkuu wa shule ahakikishe anatekeleza hili" Amesema Mkurugenzi Rwiza
Ili kuhakikisha wanafunzi wanaongeza maarifa na ustadi amewataka walimu hao kuanzisha na kuendeleza klabu mbalimbali katika shule zao akisisitiza kuwa ni mfumo mzuri wa kuwajengea uwezo pamoja na kuwaongezea maarifa wanafunzi.
Aidha katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na katika ubora tarajiwa,Mkurugenzi huyo amewataka washiriki wa kikao hiko kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha kila mmoja anatimiza majukumu yake ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi.
Rwiza amewataka Maafisa Elimu Kata, kutimiza wajibu wao wa kusimamia na kufuatilia masuala ya taaluma katika maeneo yao lengo likiwa ni kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.