Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma Ndg. Philemon Mwita Magesa, ameanzisha mpango wa kufanya kazi masaa 24 usiku na mchana ili kuhakikisha miradi ya elimu inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Mpango huu umeanza kutekelezwa katika Shule ya Sekondari Nasuli kama sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya shule.
Kwa mujibu wa DED Magesa, hatua hii inalenga kuharakisha ukamilishaji wa miradi na kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia.
“Tumeamua kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi kwa kufanya kazi masaa 24. Hii itatuwezesha kukamilisha miradi kwa haraka na kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora za elimu,” alisema.
Wakazi wa eneo hilo wamepongeza juhudi hizi, wakisema kuwa zitachangia kuinua viwango vya elimu na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.