Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Chiriku Chilumba ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta fedha kiasi cha shilingi bilioni nne kutekeleza ujenzi wa sekondari ya wasichana Mkoa wa Ruvuma iliyopewa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan iliyojengwa wilaya ya eneo ;a Migelegele wilayani Namtumbo.
Chilumba amesema ofisi yake inasimamia miradi yote ukiwemo mradi wa sekondari ya Mkoa wa Ruvuma ya wasichana ili mradi huo itekelezwe Kwa kiwango kinachostahili na sio vinginevyo alisema Chilumba.
Naye Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Michael Lyambilo alisema Shule hiyo Kwa mara ya kwanza imefunguliwa mwaka huu na kupangiwa na Serikali kupokea wanafunzi 249 na walioripoti na kuendelea na masomo ni wanafunzi 200
Hata hivyo Lyambilo amesema shule hiyo ina miundombinu mizuri kiasi ambacho kinarahishia wanafunzi wa shule hiyo kuwa na mazingira mazuri ya kupata elimu alisema Lyambilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.