Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Ndg. Philemon Mwita Magesa, ameshiriki katika mafunzo maalum kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji, yaliyoandaliwa na Halmashauri hiyo kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Mafunzo haya yamelenga kuwawezesha viongozi wapya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu.
Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, wilayani Namtumbo, yakihusisha wawakilishi wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo Mkoani Dodoma . Viongozi walipewa mwongozo wa utendaji bora ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Philemon Mwita Magesa aliwasisitiza viongozi hao kuzingatia maadili ya uongozi, uwajibikaji na ushirikiano na wananchi katika kuleta maendeleo. Aliwataka kutumia maarifa waliyopewa kuboresha utawala bora kwenye maeneo yao, akisema:
“Ni jukumu letu kuhakikisha tunawatumikia wananchi kwa haki, uwazi na uadilifu. Viongozi wa vijiji na vitongoji ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi, hivyo mnapaswa kuwa mfano wa uongozi bora kwa jamii mnayoiongoza.”
Mafunzo haya yameacha alama muhimu kwa viongozi wa vijiji na vitongoji, ambao wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa bidii na uaminifu kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Namtumbo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.