Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Khalid Khalif amewataka Watumishi wa Afya kutoa Huduma Bora kwa wananchi,kwa kuwahudumia na kutumia Mfumo wa GOTHOMIS katika Vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya.
Khalif ametoa maelekezo hayo katika ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za watumishi katika Kituo cha Afya Mbamba bay, Kihagara na Zahanati ya Mbuyula.
Bw Khalif amefafanua kuwa watumishi wa Sekta ya Afya ni wafanyakazi muhimu wanaotatua kero za wananchi,ambapo amewashauri kuwa wakarimu,wanaomsikiliza mteja,na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
“Nachukua fursa hii kuwasihi watumishi wenzangu, kuwahudumia wananchi kwa viwango vya hali ya juu, ili kuchochea maendeleo, hivyo basi ninawaagiza mtoe huduma bora kwa wananchi na wananchi wafurahie huduma zenu”,alisem..
Ameagiza wananchi wanapofika katika Vituo vya afya wapokelewe na wahudumiwe Vizuri kwa lengo la kutoa huduma bora na kupunguza malalamiko ya wananchi.
Hata hivyo amemwagiza Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Dkt John Mrina kuhakikisha huduma zote za afya zinatolewa kwa Mfumo wa GOTHOMIS kuanzia mteja anapopokelewa hadi anapoishia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.