Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa Khalid Khalif amewapongeza wauguzi kwa kutekeleza vizuri majukumu yao ya kutoa huduma za afya kwa wananchi.
Akizungumza na wauguzi,katika Hospitali ya wilaya ya Nyasa amewapongeza wauguzi kwa kufanya matendo ya huruma na kwa wagonjwa.
Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw.khalid Khalif.
Khalif amewataka wauguzi kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma Bora kwa wananchi, Ili kutatua changamoto ya afya na kuboresha sekta hiyo katika ngazi ya wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
“kazi ya uuguzi ni kazi nyeti, ambayo inasimamia Afya, hivyo Kila muuguzi anatakiwa kusimamia kiapo chake, kwa kutoa huduma bora kwa wananchi, Ili wawe na imani na Serikali katika sekta ya afya’’,alisema.
Ameongeza kuwa Serikali imefanya maboresho makubwa katika sekta ya afya, kwa kujenga miundombinu ya majengo ya kununua vifaa tiba.
Ametoa wito kwa wauguzi kuchapa kazi kwa bidii wakati Serikali inaendelea kutatua changamoto zinazowakabili.
Hata hivyo amesema Wilaya ya Nyasa inaendelea kutatua changamoto za watumishi wa sekta ya afya kwa kuomba kibali Cha kuajiri wauguzi na kujenga hoja ya watumishi wasiopandishwa madaraja kwa muda mrefu ili wapandishwe kwa mseleleko.
Awali wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi, wauguzi wamesema wanachangamoto ya kuchelewa kupanda Madaraja, upungufu wa nyumba za wauguzi,na kutolipwa kazi ya ziada.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.