Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma Ndg. Chiza Marando, ameendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyopangwa.
Katika ziara yake, DED Marando alikagua ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Mchoteka, mradi unaogharimu shilingi milioni 256, ambao uko katika hatua za umaliziaji.
Aidha, alikagua ujenzi wa matundu sita ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 10 na laki 2, ambayo yapo katika hatua ya upauaji. Miradi hiyo inalenga kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumza katika ukaguzi huo, DED Marando aliwataka wataalamu, wasimamizi wa miradi, na wakandarasi kuhakikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo unafanyika kwa ubora na unakamilika kwa wakati. Alisisitiza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unapaswa kuzingatia viwango vilivyopangwa ili wananchi wanufaike na huduma bora za maendeleo.
Pia, aliwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imetoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi zinazoboresha miundombinu ya elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.