Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma Ndg. Chiza C. Marando, ameendesha ukaguzi wa miradi ya maendeleo usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyopangwa.
Katika ukaguzi wake, DED Marando ametembelea mradi wa ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Mchoteka, wenye gharama ya Shilingi milioni 256, ambao uko katika hatua za mwisho za umaliziaji.
Marandu Pia, alikagua ujenzi wa matundu sita ya vyoo yanayogharimu Shilingi milioni 10.2, ambayo yapo katika hatua ya upauaji.
Akiwa katika ziara hiyo, DED Marando amewataka wasimamizi wa miradi na wakandarasi kuhakikisha kazi inatekelezwa kwa viwango vya juu na kukamilika kwa wakati. Aidha, amesisitiza ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.