Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Ndugu Chiza Marando, amefikia makubaliano na wafanyabiashara wa Soko la Tudeco na Soko la Generation kuhakikisha wanaanza rasmi biashara katika maeneo hayo ifikapo tarehe 1 Machi 2025.
Makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao kilichofanyika katika ofisi yake mjini Tunduru.
Aidha, Mkurugenzi amemtaka Mwanasheria wa Halmashauri kuweka mikataba ya makubaliano ili kuhakikisha kuwa kuanzia tarehe 1 Machi 2025, wafanyabiashara hao wanaanza kulipia kodi hata kama bado watakuwa hawajakamilisha marekebisho ya vibanda vyao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.