Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt Charles Msonde akimpongeza mwananchi wa kijiji cha Upolo Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Fredirick Milinga ambaye ametoa bure hekari 11 zenye thamani ya zaidi ya milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Kata ya Upolo ambapo serikali kupitia program ya SEQUIP imetoa shilingi milioni 560 kutekeleza mradi wa shule hiyo.
Dkt Msonde amekagua mradi huo ambapo ameagiza hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu mradi huo uwe umekamilika kwa asilimia 100.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya kutembelea miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa mkoani Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.