Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesisitiza umuhimu wa maandalizi ya rasilimali watu ili kukuza uchumi wa nchi ambapo amesema ni muhimu kutoa maarifa na ujuzi kwa watu wote ili kuleta ustawi katika jamii.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu wazima, ambayo kimkoa imeadhimishwa Wilayani Nyasa, Bi. Mary amesema Nchi yoyote duniani bila kuwa na rasilimali watu ambayo imeandaliwa vema, vigezo vingine haviwezi kuwa na manufaa na maendeleo yanaweza kuwa ni ndoto.
Amebainisha kuwa bado jitihada zinahitajika ili kuongeza idadi ya wanafunzi na kuimarisha Elimu ya watu wazima kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila msichana aliyekatisha masomo anarejeshwa shuleni.
“Niwaombe ndugu zangu wa Taasisi ya Elimu ya watu wazima Mkoa wa Ruvuma kusimamia uwepo wa madarasa ya kutosha kupitia mradi wa SEQUIP na kuona umuhimu wa mtoto wa kike anamaliza masomo yake licha ya changamoto anazopitia,” alisema Bi. Mary.
Bi. Mary ametoa rai kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma, maafisa Elimu msingi na sekondari kuhakikisha kuwa Elimu ya watu wazima inatiliwa mkazo kwa kuweka mikakati mizuri ili iweze kutekelezwa vizuri zaidi ya hivi sasa.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe. Peres Magiri amewataka wanafunzi waliopo katika mradi wa Elimu ya watu wazima kuitumia fursa hiyo vizuri kwa kuwa wanaweza kufanya vizuri na kuwa msaada mkubwa katika maisha yao na jamii kwa ujumla.
Amewashukuru wadau wa Elimu wanaoshirikianana nao na kuwasisitiza wote wanaoshiriki mradi huo ikiwa ni pamoja na walimu kuendelea kutimiza wajibu wao.
Juma la Elimu ya watu wazima ni maadhimisho ya kusherehekea maendeleo na mafanikio ya Elimu ya watu wazima nchini na kufanya tathmini ya shughuli za Elimu ya watu wazima zinazotekelezwa kwa kipindi cha mwaka mzima.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.