• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

ELIMU yapunguza madhara ya tembo kwa wananchi Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: April 18th, 2024

Diwani wa kata ya Likuyu Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kassimu Gunda amewashauri viongozi wa Serikali Kuwajenga wananchi kisaikolojia kwenye migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Likuyu,Gunda amesema ipo tabia ya viongozi kutojitokeza kwenye migogoro kati ya wanyamapori na binadamu hasa inapotokea binadamu kuuawa na tembo kwa kuogopa Wananchi kuwa na hasira Kwa viongozi wao.

Gunda ameitaja faida ya viongozi kuwa na wananchi wakati wa matatizo yao kunawajenga wananchi kisaikolojia  hivyo kushirikiana nao bega Kwa bega kwenye changamoto mbalimbali .

Diwani huyo ameiomba serikali Kuharakisha kifutajasho kwa wananchi pale wanapoathirika na tembo ili wananchi walioathirika na wanyamapori waweze Kununua chakula ambacho kiliharibiwa na wanyamapori hao.

Hata hivyo Menas Fusi Mkazi wa kitongoji cha Mfuate Kijiji Cha Likuyu amesema kasi ya tembo kwenda katika mashamba ya wakulima imepungua Kutokana na kuwepo Kwa Jeshi la TANAPA ambalo Kwa kiasi kikubwa hufanya kazi ya kuwarudisha tembo hao katika hifadhi .

Afisa Maliasili na Utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Priska Msuha amesema Licha ya kutokea Changamoto ya tembo mmoja mwenye mtoto kumua mwananchi katika Kijiji Cha Likuyu hivi karibuni, changamoto ya tembo imepungua Kutokana na Kambi ya TANAPA kufanya kazi kubwa ya kuwarudisha wanyamapori hao hifadhini.

Afisa Maliasili huyo amesema ofisi yake inaendelea kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na wanyamapori kama tembo ambapo hivi sasa wananchi wakimwona tembo hawamfuati hubaki kimya badala yake wanapiga simu  kwa Mamlaka zinazohusika ambao hufika kuwaondoa tembo hao katika makazi ya watu.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.