HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma imezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa watoto wa shule za msingi na Sekondari wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi14.
Zoezi hilo limezinduliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed aliyewakilishwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Philemoni Namwinga katika Shule ya Msingi Kifaguro.
Namwinga akizungumza katika zoezi hilo amesema lengo la chanjo zote ni kujenga jamii yenye Afya, ikiwa kauli mbiu ya jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya.
Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr. Manyanza Mponeja amesema mpango wa chanjo hiyo ni kuwakinga watoto ambao hawajaanza kufanya ngono wenye umri wa miaka 9-14.
“Naomba nitoe wito kwa wazi kuhakikisha watoto wa kiume wanafanyiwa tohara salama inasaidia kupunguza maambukizi kwao hasa HIV na kuwa msafi’’,alisisitiza.
Amesema zoezi hilo litafanyika kuanzia Aprili 22 hadi 28 mwaka huu kwa kuhakikisha chanjo katika Halmashauri hiyo inafikia asilimia 80 ya watoto waliochanjwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.