HALMASHAURI ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma imepanga kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi bilioni 12 kwa ajili ya Maendeleo katika mwaka wa fedha 2021/2022.
Akizungumza katika kikao maalum cha kupitisha bajeti hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri mjini Madaba,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda amesema katika uandaaji wa bajeti wa mwaka 2021-2022,Halmashauri imezingatia miongozo na maelekezo mbalimbali ya Serikali.
Ameitaja miongozo hiyo kuwa ni ukusanyaji wa mapato na utendaji wa Rasilimali fedha, mpango wa maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2021 mpaka 2025 ambapo mpango huo unazingatia vipaumbele vya kisekta kama vile Fedha,Elimu,Mifugo,uvuvi,Afya, uthibibiti wa maji taka,Utalii na Viwanda.
“Halmashauri imezingatia katka uandaji wa bajeti 2021-2022 Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, hotuba ya Rais wa Tanzania na hotuba ya Waziri Mkuu na ziara yake ya tarehe 4 mpaka 7 Januari 2021 Mkoani Ruvuma na kuzingatia masuala mtambuka kama Magonjwa ya Ukimwi,Maafa,Mazingira na Rushwa,mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa Mkoa na Taifa”,alisema.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Teofanes Mlelwa akizungumza wakati anakifunga kikao hicho amewataka wataalamu wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi ili kuwe na tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Mlelwa ametoa rai kwa wataalam hao kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao kwa sababu bajeti imepitishwa hivyo ushirikiano wa watendaji unahitajika zaidi.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Machi 13,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.