HALMASHAURI ya Madaba Wilaya ya Songea imetoa Mkopo wa Bodaboda 5 kwa kikundi cha Kona Bar zenye thamani ya Shilingi milioni 20.
Akisoma taarifa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema kwa mwaka wa fedha 2021-20022 wamefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 20 kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 126.
Mohamed amesema vikundi 7 ni vya wanawake vilikopeshwa zaidi ya shilingi milioni 40,vikundi 8 ni vya vijana vilikopeshwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 74 na vikundi 5 vya watu wenye ulemavu vilikopeshwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 11.
“Tunatarajia kuendelea kutoa mikopo yenye tija kwa makundi maalumu na kusimamia vikundi kwa kutumia mikopo katika kuzalisha miradi waliyoombea fedha ili kujenga ufanisi mkubwa wa kurejesha mikopo kwa wakati na kupiga hatua ya maendeleo”.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amekuwa mgeni rasmi katika hafla ya ugawaji wa Bodaboda hizo amewaasa wanakikundi hao kutii sheria pamoja na kuwa na Leseni ikiwa Pikipiki hizo zimekatiwa bima kubwa.
Mgema amesema asilimia 10 inayopatikana katika mapato ya ndani ya Halmashauri zitumike vizuri kwa wanawake,watu wenye ulemavu pamoja na vijana ili waweze kutumia na kurejesha kwa wakati iliwengine waweze kupata.
”Mikopo iliyokopeshwa ni milioni 126 kwa Halmashauri ndogo ya Madaba kati ya hizo zingine ni za marejesho ya mwaka uliopita kwa kiwango hiki tunaweza kufikia milioni mia tano za kukopesha”.
Katibu wa Kikundi cha Kona Bar Erasto Filemon ameipongeza Serikali kwa kuwapatia Mkopo huo na ameahidi kusimamia kikundi hicho kurejesha kwa wakati ikiwa ni mkopo wa pili na kupitia mkopo huo wamepata manufaa kwa kuwainua kimaisha vijana wa Madaba.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Mai 12,2022
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.