• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

HALMASHAURI ya Mbinga ilivyosimamia uandkishaji daftari la wapigakura

Imewekwa kuanzia tarehe: October 21st, 2024

WATUMISHI wa Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma,wamelazimika kutoka ofisini na kwenda kupiga kambi katika vijiji mbalimbali  ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha  katika Daftari la wapiga kura.

Halmashauri  hiyo imefikia uamuzi huo  ili kuhakikisha hakuna mwananchi mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anakosa  nafasi ya kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Andrew Mbunda wakati akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura katika vituo mbalimbali wilayani humo.

Amesema,zoezi la uandikishaji wapiga kura linakwenda vizuri  na kuna mwitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza na hadi sasa zaidi ya asilimia 92 ya wamejiandikisha katika vituo 782 vilivyotengwa katika Halmashauri hiyo.

Mbunda amesema,mwitikio huo umetokana na wananchi kupewa elimu kuhusu umuhimu wa kujiandikisha na uhamasishaji unaofanywa na watumishi wa ngazi mbalimbali za Halmashauri wakiwemo watendaji wa vijiji na kata na matangazo yanayotolewa kila siku kwenye vijiji na vitongoji.

Amesema,ili kufikisha lengo la asilimia 100 la uandikishaji na kupata takwimu sahihi za  wapiga kura katika uchaguzi huo,Halmashauri imeweka utaratibu ambapo kila kitongoji,kijiji na kata zenye jukumu la kutambua wakazi wake na wale wenye sifa  wanahamasishwa kwenda kujiandikisha ili waweze kushiriki katika uchaguzi huo.

“Tumebakiwa na siku moja kabla ya kufunga zoezi la uandikishaji,tunaamini asilimia 8 iliyobaki tutaifikia kutokana na mikakati kabambe tuliyojiwekea katika Halmashauri yetu,tumeongeza nguvu ili kuwafikia watu wote wenye sifa ya kupiga kura siku ya tarehe 27 mwezi ujao”alisema Mbunda.

Pia alisema,katika utekelezaji wa zoezi hilo changamoto kubwa ilikuwa uelewa mdogo wa wananchi kwani siyo wote waliotambua umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura.

Kwa mujibu wa Mbunda ni kwamba,awali wananchi  walidhani wakifika kwenye vituo watatumia muda mrefu kujiandikisha,lakini wanapofika kwenye vituo wanakuta hali ni tofauti kwani wanatumia muda mchache, hivyo wale ambao hawajajiandikisha wanakwenda kwenye vituo vilivyotengwa.

“Hofu kubwa ya wananchi walidhani wakifika watapoteza muda wao  wa siku nzima wakiwa vituoni,kumbe hali ni tofauti kabisa kwani ukifika kituoni mwandikishaji atakuuliza majina matatu,umri na kusaini kwa kidole gumba au kwa peni tu na siyo vinginevyo”alisema Mbunda.

Mbunda,Namevishukuru vyama  vyote vya siasa kwa  kazi nzuri ya kuhamasisha wanachama wao kwenda kujiandikisha na kuwaomba waendelee na uhamasishaji huo hadi siku ya kupiga kura tarehe 27 mwezi Novemba mwaka huu.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.