Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma itaendelea kushirikiana na mashirika ya kidini katika kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya hususan huduma ya mama na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura katika kikao cha tathmini ya makubaliano ya utoaji wa huduma za afya baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Jimbo Katoliki la Mbinga kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2023.
Mkurugenzi Kashushura amebainisha kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa mashirika ya kidini katika kutoa huduma bora za afya nchini.
“Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na mashirika ya kidini ni ahidi kwamba ushirikiano huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga utakuwa endelevu”
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Mbinga John Ndimbo amemuomba Mkurugenzi Kashushura kusaidia kutatua changamoto ya upungufu wa watoa huduma za afya katika Hospitali ya Litembo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ili hospitali hiyo iendelee kutoa huduma bora na kuwafikia wananachi wengi zaidi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.