Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imekuja na mkakati wa ujenzi wa hosteli katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambayo itatoa huduma kwa wananchi ambao wamewaleta ndugu zao kuja kupata huduma za afya katika hospitali hiyo.
Utekelezaji huo ni chanzo cha mapato ya ndani ya Halmashauri utaondoa adha kwa wananchi ambao wanalazimika kutafuta malazi maeneo mbalimbali ambayo yapo mbali na hospitali hiyo.
Mkakati huo umebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura katika ziara yake ya kutembelea Hospitali hiyo kukagua utoaji wa huduma za afya pamoja na ujenzi wa wodi tatu unaoendelea kutekelezwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.