Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imepokea shilingi 2,242,211,308 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa shule nne mpya za sekondari katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Shule hizo zimejengwa katika kata za Nyoni, Litembo, na Muungano, ambapo tayari zimekamilika na zimeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza tangu Januari 2025.
Shule moja inayoendelea kujengwa iko katika Kata ya Langiro, na ujenzi wake unaendelea.
Kaimu Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Rashid Bundalah, alibainisha kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wazazi ambao watoto wao hawajaripoti shule ndani ya wiki moja kuanzia tarehe 15 Machi 2025.
“Tunaona jinsi Serikali inavyowekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule, lakini bado kuna wazazi wamekaa na watoto majumbani. Hii si sawa, tunapaswa kuunga mkono jitihada za Rais wetu,” alisema.
Katika hatua nyingine ya kuboresha elimu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ilipokea walimu 36 wa masomo mbalimbali mwezi Februari 2025, na tayari wameripoti katika vituo vyao vya kazi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.