HALMASHAURI ya wilaya Nyasa mkoani Ruvuma,imefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo
ya mapato yake ya ndani baada ya kukusanya Sh.bilioni 1.824 sawa na asilimia
104 kati ya lengo la kukusanya Sh.bilioni 1.7.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Khalid Khalif alipokuwa
akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kikao cha Baraza la
madiwani.
Amesema,kwa mwaka 2023/2024 Halmashauri ya wilaya Nyasa ilipokea
Sh.bilioni 9,018,973,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
kati ya fedha hizo Sh.bilioni 4,664,725,000.00 ni fedha za ndani na Sh.bilioni
4,364,248,000.00 ni fedha za nje.
Kwa mujibu wa Khalif Sh.milioni 181,120,000.00 sawa na asilimia 20 zimetengwa
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka mapato ya ndani ya
Halmashauri hivyo kufanya jumla ya fedha zilizotengwa kuwa Sh.bilioni
9,200,093,000.00.
Amesema,kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri imeongeza ukomo wabajeti
ya makusanyo ya ndani kwa zaidi ya asilimia 50 kufikia Shilingi bilioni 2.4.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Khalid Khalifa akizungumza kwenye Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo mjini Mbamba baya
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.