SERIKALI imetoa zaidi ya shilingi milioni 226 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kutekeleza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD na matundu ya vyoo 17 katika shule ya msingi Ukuli Kata ya Kingerikiti.
Akitoa taarifa ya miradi hiyo kwa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Jimson Mhagama amesema serikali imetoa kiasi cha sh.milioni 200 kujenga OPD na matundu sita ya vyoo katika kituo cha Afya Kingerikiti.
Mhagama amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Aprili 24 mwaka huu na unatarajia kukamilika Agosti 30 mwaka huu ambapo mradi upo katika hatua ya jamvi ukiwa na asilimia 25 na hatua ya lenta ni asilimia 47 na kwamba mradi unatekelezwa kwa force akaunti.
“Eneo la mradi lina ukubwa wa hekari 18,hadi sasa mradi umetoa ajira za muda kwa watu 30,mradi unatekelezwa kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Kingerikiti kutoka vijiji vinne vya Kingerikiti,Ukuli,Lumecha na Mawasiliano.
Akizungumzia mradi wa matundu 17 ya vyoo katika shule ya msingi Ukuli,Mkurugenzi huyo amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 26 kupitia fedha za udhamini kutoka SWASH kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo.
Amesema utekelezaji wa mradi huo ni kwa kutumia force akaunti na kwamba mradi umeanza Juni 3 mwaka huu na ulitarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka huu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Nuru Ngeleja amewapongeza wananchi wa kijiji cha Ukulu kwa kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya vyoo ambavyo amesema vitawawezesha wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kuwa na mazingira rafiki ya kusomea na kulinda afya zao.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu Mhagama ameipongeza serikali kwa kuamua kujenga kituo cha Afya Kingerikiti ambacho amesema kitakuwa ukombozi wa wananchi hao ambao walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Musa Homera amewapongeza watendaji wa Halmashauri ya Nyasa kwa kusimamia vema miradi ya maendeleo ambayo mingi imekamilika na imeanza kuwanufaisha wananchi.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Juni 5,2020
Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.