Divisheni ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, imeanza Kampeni ya kitaifa ya Chanjo kwa siku tano kwa watoto wa kike dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.
Chanjo hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya virusi vinavyoitwa (Human Papilloma Virus) HPV ambavyo vinasababisha saratani ya Mlango wa kizazi kwa wanawake.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dr.Geofray Kihaule amewataja Waathirika zaidi wa ugonjwa huo ni wanawake na kwamba Chanjo hiyo inatolewa kwa watoto kati ya miaka 9 hadi .
Amesisitiza kuwa Chanjo hiyo inatolewa ni bure haina malipo yeyote ambapo ametoa rai kwa wazazi wasisite kuwapeleka watoto wao kupata chanjo na kwamba chanjo hiyo haina madhara yeyote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.