TAASISI isiyo ya kiserikali ya RUATI imehitimisha mafunzo ya kilimo biashara ambayo yamefanyika siku mbili kwa wanakundi cha wanawake wa katoliki (Karismatiki) katika ukumbi wa Mshangano Songea, mkoani Ruvuma
Akizungumza baada ya kuhitimisha mafunzo hayo mratibu wa Rural and Urban Agricultulral Tenchnology Initiatives (RUATI) Mkoa wa Ruvuma Mohamed Waziri alisemesa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo waweze kuzalisha kwa tija.
“Tunachofanya ni kuwaelewesha njia bora za uzalishaji pamoja na matumizi sahihi ya mbolea lakini vile vile matumizi sahihi ya mbegu bora ambazo zinafanya azalishe kwa tija kwa eneo dogo pia apate kiasi kikubwa cha mazao”, alisema Waziri.
Mmoja wa wanakikundi hicho, Mariana Kiwili alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wakulima inafaida kubwa kwani inamjengea Mkulima uwezo wa kujua njia sahihi za kilimo na kuacha kulima kwa mazoea.
“Kwa kweli tumefurahi kupata mafunzo haya maana tulikuwa tunalima kwa njia ambayo ilikuwa sio bora na kupelekea kupata mazao machache na tunaamini mwaka huu utakuwa ni mwaka wa mavuno mengi baada ya kupata elimu kwenye mafunzo haya” alisema Kiwili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.